Feb 22, 2015

MWADUI FC YA JULIO BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA

Bao pekee lililofungwa na Kelvin Sabato limeiwezesha Mwadui FC kuibuka na ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza.

Mwadui FC chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imeibuka na ushindi wa bao hilo dhidi ya African Sports ya Tanga na kutawazwa kuwa bingwa katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.
SABATO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO HILO PEKEE. KULIA NI BAKARI KIGODEKO AKIMPONGEZA.
Mechi hiyo iliwakutanisha vinara wa makundi ya daraja la kwanza ambao walikuwa wameishajihakikishia kucheza Ligi Kuu Bara mwaka.

Julio anayeaminika kuwa kocha mwenye maneno mengi, kikosi chake kilijitahidi kupamba na kasi ya Sports ambayo ilikuwa inaundwa na vijana wengi.
Soka lilikuwa safi na la kuvutia huku Mwadui ikitawala zaidi kutokana na wakongwe wake, Athumani Iddi ‘Chuji’, Juma Jabu, Bakari Kigodeko na wengine kuonyesha soka safi.

Hata hivyo, African Sports yenye vijana wengi pia ilionyesha soka safi.
 Mshambuliaji Ally Shiboli wa Sports naye alikuwa msumbufu sana kwa mabeki wa Mwadui lakini akatoa kali baada ya kumpiga kipa chenga lakini akashindwa kufunga akiwa amebaki na lango.




0 maoni:

Post a Comment