Feb 22, 2015

PRISONS YAITULIZA AZAM CHAMANZI

Sare ya bila kufungana dhidi ya Prisons ya Mbeya imezidi kuibana Azam FC.

Sasa imefikisha pointi 27 baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, leo.

Yanga inaendelea kuongoza ikiwa na pointi nne zaidi ya Azam FC ikiwa ni baada ya kuitwanga Mbeya City kwa mabao 3-1.

Azam imecheza mechi 15, imeshinda saba, sare sita na wamepoteza mbili.

0 maoni:

Post a Comment