Mar 8, 2015

ALICHOSEMA JULIO BAADA YA JANA KULAZIMISHWA SARE NYUMBANI


kagera sugarNa. Richard Bakana
Kocha msaidizi wa klabu ya Coastal Union, kutoka Tanga, Jamhuri Kihwero ‘Julio’ ameangushia zingo la lawama safu yake ulinzi na kusema kuwa wamecheza kipuuzi kitu kilichopelekea kugawana pointi moja moja na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzamia bara uliomalizika kwa sare ya 2-2 Mkwakwani.
Akizugumza na Shaffihdauda.com baada ya mchezo huo,  alisema kuwa tayari mchezo huo walikuwa wameuweza, lakini kutokana na makosa yaliyofanywa na mabeki, Kagera Sugar waliweza kusawazisha licha ya Coastal Union, kuongoza kwa bao moja  hadi dakika 45 za mwanzo zinamalizika, kufatia kazi safi ya Seleman Kibuta aliyemalizia mpira uliokuwa ukizagaa katika lango la Kagera ikiwa ni dakika ya 6 ya mchezo.
“Mimi nasema hapa hakuna swala la Ufundi kwasababu wamepoteza umakini, Mchezo tulikuwa tumeshinda tayari, zilikuwa zimebaki dakika kama saba wameruhusu goli la kipuuzi ambalo kila mtu kwa kweli limemuuzi, Na hii ni kukusekana kwa umakini kwa sababu Kagera hawakuweza kukata tamaa, wameweza kushambulia wakitaka kurudisha na wamewez, Kwahiyo ni uzembe wa mabeki wetu, Mara ya kwanza walikuwa wanalalamika kuwa hawafungi kwahiyo kama wanafunga basi mabeki ndio watakuwa na matatizo, Tutalifanyia kazi ili kuona kwanini wanaruhusu magoli ya kizembe” Amesema Julio ambaye ni Kocha mkuu wa Mwadui FC ambayo imepanda ligi kuu msimu huu lakini Costal Union akifundisha kwa muda.
Baada ya Coastal kufanikiwa kuongoza kwa dakika 45 za mwanzo, Kagera walirudi katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga wakiwa na presha kubwa wakisaka bao ndipo Mshambuliaji Atupele Green akaisawazishia timu yake bao akiunganisha kwa kichwa krosi safi kutoka kwa Salum Kanoni na kumuacha mlindamlango wa Coastal Union Shaaban Kado akiwa hana cha kufanya ikiwa ni dakika ya 52 ya mchezo.
Katika Dakika ya 60, mwamuzi wa mchezo huo kutoka Mtwara, David Paul, aliizawadia Coastal Union, penati ambayo ilizamishwa kambani na Rama Salum, Raia wa Kenya, baada ya Abuu Mtilo kuunawa mpira ndani ya chumba cha kupigia penati, na kufanya Wagosi hao wa kaya kufikisha bao 2-1.
Pongezi ziende kwa Rashid Mandawa aliyeisawazishia Kagera Sugar bao 2 na kufanya kibao kiwe 2-2 ikiwa ni dakika ya 84 akitumia makosa wa mabeki wa Coastal Union ambao walishindwa kuosha mbele mpira uliokuwa unazagaa katika lango lao.
Hata hivyo hadi kipenga cha mwisho kinapigwa kuashiria mtanange huo kumalizika timu hizo zikigawana pointi moja moja kwa kutoa sare ya 2-2, Wenyeji wa mchezo huo Coastal Union walimaliza wakiwa Pungufu kufatia mchezaji Othuman Tamimu kuzawadiwa kadi Nyekundu katika dakika ya 73 kwa kosa la kuchelewesha mpira ambapo tayari awali alikuwa na kadi ya njano.

0 maoni:

Post a Comment