Di
Maria hajaonyesha umahiri wake tangu aliposajiliwa katika kilabu ya
Manchester united kutoka Real Madrid na inaaminika kwamba yeye na mkewe
hawajazoea maisha ya Manchester baada ya jaribio la wizi katika nyumba
yao.
Wiki iliopita raia huyo wa Argentina ,mkewe Jorgelina Cardoso
na mwanawe wa mwaka mmoja wamehamia katika nyumba ya aliyekuwa mchezaji
wa Manchester United Phil Nevile iliopo ghorofa ya 45.Wamekodisha nyumba hiyo kwa kuwa Di Maria ana mpango m'badala wa maisha yake swala ambalo kilabu ya Manchester United inalifahamu.
Hatua hiyo inadaiwa kushinikiza harakati za kilabu hiyo kutaka kumsajili mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale.
Ijapokuwa Bale amekuwa akisema kuwa hataki kuondoka katika kilabu ya Real Madrid ili kurudi katika ligi ya Uingereza,United inahisi kwamba inaweza kum'bembeleza ili kubadilisha msimamo wake iwapo watakubaliana na mabingwa hao wa Ulaya.
0 maoni:
Post a Comment