TIMU
ya Real Madrid imefungwa 1-0 na Athletic Bilbao Uwanja wa San Mames
usiku huu na maana yake iwapo Barcelona itaifunga Rayo Vallecano kesho
mchana itapanda kileleni mwa La Liga.
Gareth
Bale aligongesha mwamba akiwa umbali wa mita 50 kabla ya Aritz Aduriz
kufunga kwa kichwa dakika 26, bao tosha kabisa kuipa ushindi mwembamba
Athletic.
Kikosi cha
Athletic Bilbao kilikuwa: Iraizoz, Iraola, Balenziaga, Etxeita,
Gurpegui, Benat, Mikel Rico/Toquero, dk91, De Marcos, Muniain/Susaeta
dk64, Aduriz na Williams/Fernandez Hierro dk75).
Real
Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo, Illarramendi/Jese
dk71, Isco, Kroos/Borges dk76, Ronaldo, Bale na Benzema/Hernandez dk80.
Karim Benzema (kushoto) na Cristiano Ronaldo wakiwa hawaamini macho yao huku wachezaji wa Bilbao wakishangilia bao lao
0 maoni:
Post a Comment