Kuelekea mchezo wa mahasimu wa
kandanda nchini Simba SC v Yanga SC kesho Jumapili katika uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam mshambulizi aliyefunga mabao matano katika michezo
iliyopita Jerson Tegete ameuambia mtandao huu kuwa mechi hiyo itakuwa
ngumu kwa kuwa kila timu inahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi
nzuri katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.
“ Itakuwa ni mechi ngumu ambayo
kila timu inahitaji kushinda, kwa upande wetu ( Yanga) tunahitaji
ushindi ili kuelekea katika njia sahihi ya ubingwa, lakini kwa upande
mwingine ni mchezo huu ni sehemu ya sisi kujiandaa na mchezo wa kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya Platinum ya Zimbabwe. Simba pia watahitaji
kushinda ili kusogea juu ya msimamo lakini naamini Yanga
tutashinda´anasema Tegete.
Yanga ndiyo vinara wa ligi kuu
hadi sasa, wakiwa na alama 31 watahitaji kuishinda Simba ili kuwazidi
mahasimu wao hao kwa alama 11. Katika michezo minne iliyopita timu hizo
zimetoka sare huku Yanga ikiwa haijafunga goli lolote katika michezo
miwili mfululizo dhidi ya Simba ( ukiwemo mchezo wa Nani Mtani Jembe-2).
Tegete ambaye amepoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Yanga
cha Yanga ana imani hali hiyo itatoweka mara baada ya kumalizika kwa
dakika 90.
“ Naamini kila kitu kitakuwa
sawa, tutafunga safari hii, kikubwa tunaenda uwanjani ili kufunga magoli
na kuisaidia timu yetu kushinda. Kutokufunga huwa ni hali ya kawaida,
hutokea tu lakini tumejipanga kushinda. Niko fiti kama nitapata nafasi
nitacheza. Yanga hatuna hofu kuhusu game hiyo, tuko vizuri hivyo ushindi
ni hitaji letu. Natamani kucheza kwa mara nyingine katika pambano la
mahasimu hao” anamaliza kusema Tegete wakati alipofanya mahojiano na
mwandishi wa habari hii.
0 maoni:
Post a Comment