Mara nyingi binadamu
kama viumbe hai siku zote huwa tunapenda kuangalia muonekano wa mtu
kiujumla na kukadiria miaka ya mtu husika kuwa huyu atakuwa na umri
huu, wengi huangalia sura au ukomavu wa mwili halikadhalika umbo la
mtu.
Leo nimekuletea
wachezaji ambao huwezi ukadhania kabisa kama umri wao upo sawa mtu wangu
na kumekuwa na malalamiko ya wengi kuwa walidanganya umri na wengi
hawaamini miaka yao kama ipo sahihi.
1. Diego Costa na Nzuri Sahn (26 miaka)
Mshambuliaji ambaye
yupo katika kiwango cha upachikaji wa mabao kwa Chelsea hivi sasa Diego
Costa wengi wa watu hawaamini kabisa umri wake alionao sababu ya
muonekano wake kiujumla hasa muonekano wa sura yake ambayo inaobekana
kuwa ni ya kiutu uzima sana. Diego Costa alizaliwa mwaka 1989 huko
Brazil na hadi sasa ana miaka 26.
Achilia mbali
mshambuliaji huyo tunaye mwingine ambaye ni kiungo kutoka Borussia
Dortmund Nzuri Sahn naye ana miaka 26 na alizaliwa mwaka mmoja sawa na
Diego Costa wakiwa wote wana miaka 26.
Mshambuliaji aliyekuwa
katika kiwango mathubuti na cha hatari zaidi Fernando Torres wakati huo
akiwa katika majogoo wa Liverpool na baadae kutimkia Chelsea kisha
kurejea tena katika timu yake ya mwanzo Athletico Madrid alizaliwa mnamo
mwaka 1985.
Umri huo hakuna tofauti
na mshambuliaji mwingine ambaye amekuwa katika kiwango kizuri sana
akiwa na Club ya Bayern Munich kwasasa Arjen Robben, amezaliwa pia mwaka
1985 ila jinsi muonekano wake ulivyo hauwezi ukaamini kirahisi kama ana
miaka hiyo 30 maana wengi wa mashabiki na wachezaji wenzie wanadhania
anaweza akawa anafikisha miaka 40 na kuendelea ila mwisho wa siku ukweli
utabakia palepale ana miaka 30 hadi sasa.
0 maoni:
Post a Comment