Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
AZAM FC walikutana na ‘ matokeo mabaya’ kisha kuondolewa katika michuano ya CAF Champions League. IKicheza kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo, huku ikiwa ni mara ya tatu kwa klabu hiyo kucheza michuano ya vilabu Afrika tangu ilipoanzishwa mwaka 2007 na kupanda ligi kuu msimu wa 2008/09, Azam ilikutana na ratiba ngumu mwanzo tu. Ratiba dhidi ya Azam FC vs El Merreikh, na ile ya Al Hilal vs KMKM ilikuwa ni kama ‘ kuwaondoa wawakili wa Tanzania’ na kuzipitisha timu zenye mvuto wa michuano hiyo kutoka nchini Sudan Kaskazini.
Azam walishinda ushindi wa ‘ wastani’ dhidi ya Merreikh katika uwanja wa nyumbani, ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Azam Complex wiki mbili zilizopita uliambatana na maandalizi ya hukakika. Baada ya kufungwa 3=0 katika uwanja wa Al Merreik, Khartoon, Sudan, Azam wameshusha lawama zote kwa waamuzi. Mwamuzi raia wa Zambia analalamikiwa kwa namna alivyokuwa akitoa uamuzi wa upande mmoja ikiwemo ‘ kiki ya penalti’ iliyochezwa na kipa Aishi Manula katika kipindi cha kwanza.
Umefika wakati sasa wa Azam FC kusahau matokeo hayo na kurudisha akili katika michezo ya ligi kuu ili wafanikiwe kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine mwaka ujao. Kucheza dhidi ya Merreik katika michuano yako ya kwanza ya klabu bingwa si ratiba rahisi licha ya wengi kuiweka Azam katika ‘ tawi la klabu shindani Afrika Mashariki na Kati’. LIcha ya kuondolewa katika michuano, Azam FC wanatakiwa kubaki na funzo ya kile kilichowakuta Khartoon na kuchukulia ni sehemu ya mafanikio kwa klabu zote zenye malengo makubwa Afrika.
Merreikh na mahasimu wao wa soka la Sudan, Al Hilal mtazamo wao katika michuano ya vilabu Afrika ni kucheza walau ‘ Ligi ya Mabingwa’. Kuondolewa katika hatua yoyote ile nje ya nane bora ni kufeli kwa malengo yao. Kabla ya kutoka kwa ratiba ya michuano Azam FC ilikuwa na malengo makubwa, nafikiri walikuwa sawa kabisa kuwa na mtazamo wa kufika nane bora ama hatua ya 16 bora, lakini baada ya ratiba kupangwa matuaimi hayo yalitegemea zaidi matokeo ya gemu mbili dhidi ya Merreikh.
Kuishinda timu hiyo ya Sudan kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza ni kitendo ambacho kinaikomoza haraka timu yoyote katika michuano ya kimataifa. Merreikh walikuwa na hofu dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania mara baada ya kupangwa kwa ratiba ndiyo maana waliamua kufanya maandalizi ya uhakika kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Qatar huko walicheza na klabu kubwa za Ulaya kama Schalke O4 ya Ujerumani. Wameacha funzo lingine kwa Azam FC kuwa katika michuano ya kimataifa ni lazima ufanye maandalizi makubwa nay a muda mrefu bila kujali unacheza na timu gani.
AZam wameshindwa kufunga walau goli moja ugenini ikiwa na washambuaji wa kimataifa, Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na Brian Majwega, bado natafakari matokeo yao lakini naendelea kujifunza kuwa klabu za Tanzania zinahitaji kujifunza zaidi kuhusu ‘ fitna za nje ya uwanja’ kama zinahitaji kufanya vizuri barani Afrika . Simba iliifunga Al Ahyl Shandy ya Sudan kwa mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Shirikisho mwaka 2012, wakacheza dakika 45 ugenini bila kuruhusu bao lakini baada ya dakika 90 matokeo yakawa Shandy 3-0 Simba na hivyo mechi ikaamuliwa kwa mikwaju ya penalti na Simba ikashindwa na kuondolewa.
Kwa nini walifungwa mabao 3-0 ndani ya dakika 35 za mwisho?. Wakati mwingine waamuzi ni tatizo lakini bado klabu zetu zinashindwa ugenini kutokana na kurudia makosa yale yale tu. Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Azam FC walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lakini baadaye wachezaji wakaanza kupoteza umakini na kujikuta wakifungwa. Michuano ya Tatu Afrika,
Azam FC waendelee kujifunza na kuchukulia vichapo vya Rabat, 2013, Nampula, 2014 na Khartoon, 2015 kama sehemu ya kujiimarisha nag emu muhimu za marejeano. Waliishinda FR Rabat ya Morocco kwa bao 1-0 Dar es Salaam, waliishinda Fereviarrio de Nampula kwa bao 1-0 Dar es Salaam, kisha wameifunga El Merreikh 2-0 Dar es Salaam, lakini walipoteza michezo yote ya ugenini na kuondolewa mashindanoni.
CHANZO SHAFFIHDAUDA.COM
0 maoni:
Post a Comment