Azam FC imetangaza kumfukuza kazi Kocha Joseph Omog raia wa
Cameroon.
Pamoja na Omog, Msaidizi wake, Ibrahim Shikanda ametimuliwa na
mikoba amepewa George Best Nsimbe raia wa Uganda ambaye ni msaidizi wake namba
moja.
ALIVYOKARIBISHWA NA UONGOZI WA AZAM FC, MWENYEKITI WA AZAM FC, SAID AKIMKARIBISHA. |
Best ambaye ameanza kazi Azam FC msimu uliopita, sasa ndiye ataongoza jahazi.
Ingawa uongozi wa Azam FC haujaanika kila kitu, lakini inaonekana Omog anaondoka baada ya Azam FC kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mabao jumla ya mabao 3-2.
Azam FC ilianza kwa kushinda 2-0 jijini Dar lakini ikakubali kipigo cha mabao 3-0 jijini Kharthoum.
Omog ndiye aliyeipa Azam FC ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara na ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika .
0 maoni:
Post a Comment