Mar 3, 2015

KOPUNOVIC AKATAA MECHI YA KIRAFIKI YA USIKU HUKO ZANZIBAR


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amekataa kikosi chake kucheza mechi ya kirafiki usiku.


Wanachama wa Simba walio Zanzibar walikuwa wametafuta mechi ya kirafiki baada ya ombi la kocha huyo lakini ikaonekana inatakiwa kuchezwa usiku.

Kopunovic amechukua uamuzi wa mechi hiyo kwa kusema wao na Yanga Jumapili watacheza jioni, hivyo asingependa kikosi chake kucheza mechi jioni.

Alipozungumza na SALEHJEMBE, Kopunovic alisema mechi ya kirafiki ni maandalizi ya mechi iliyo mbele yao.

"Hauwezi kucheza mechi ya kirafiki usiku halafu ucheze mechi unayojiandaa jioni. Katika uchezaji suala la mazingira pia ni muhimu sana," alisema Kopunovic.

Kocha huyo Mserbia amekuwa akiendelea na mazoezi huku akisaidiana na msaidizi wake, Selemani Matola wakijiwinda kutaka kuitwanga Yanga katika mechi ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment