Mar 3, 2015

YANGA WAZUA JIPYA KUHUSU AJIBU, WASEMA HAKUPASWA KUCHEZA

Yanga wameibuka na jipya huku wakimtaja mchezaji wa Simba Ibrahim Ajibu hakupaswa kucheza mechi dhidi ya Prisons ambayo alifunga bao tatu au hat trick.


Yanga wamesema Ajibu alikuwa na kadi tatu, lakini Simba walimchezesha kutumia kanuni ambazo bado hazijapitishwa.

Kanuni hizo ni zile zinazoiruhusu timu kuchagua mechi gani mchezaji wake akose na ipi acheze hata akiwa na kadi za njano tatu.

“Kanuni hizo bado hazijapitishwa, lakini Simba wamezitumia. Kama ni haki, basi Ajibu hakupaswa kucheza mechi ile.

“Hilo liko wazi, bodi ya ligi inajua lakini imekaa kimya na Simba wamefanya wanachotaka,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro.

Katika mechi dhidi ya Prisons, Simba ilishinda kwa mabao 5-0 huku Ajibu akitupia bao tatu peke yake.


Ushindi huo ndiyo mkubwa zaidi kwa Simba msimu huu, hali ambayo angalau imeamsha matumaini kwa mashabiki wake.

0 maoni:

Post a Comment