Mar 3, 2015

PLUIJM AFURAHIA SIKU SABA ZA MAANDALIZI DHIDI YA SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wiki moja ya maandalizi kwa ajili ya Simba, itawasaidia sana.

Yanga inaivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara utakayopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Tayari Yanga iko kambini mjini Bagamoyo ambako ilipitiliza moja kwa baada ya kutua nchini ikitokea Botswana.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Pluijm amesema kuwa wiki moja itawasaidia kurekebisha makosa kadhaa.
“Makosa hayaishi katika mpira, lakini wiki moja ya maandalizi itatupa nafasi nzuri.
“Ukiona timu imecheza vizuri ujue mlichojifunza mmekifanyia kazi, mkishindwa kufanya vizuri utaona kuna sehemu mmepungukiwa.
“Soka ni lazima urudie kujifunza, leo, kesho na siku nyingine. Hivyo siku zaidi ya tano, zitasaidia kufanya marekebisho kwa maneno na mafunzo ya vitendo,” alisema.

Yanga imecheza mechi ya mwisho dhidi ya BDF XI ya Botswana na kufanikiwa kuitoa katika Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 3-2.

0 maoni:

Post a Comment