Na Sanula Athanas
FIFA imesema inaushughulikia utata uliojitokeza kuhusu usajili wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi katika klabu za Tanzania na Tunisia.
Katika taarifa yake kwa NIPASHE jana saa 8:04 alasiri, Ofisa
Habari wa FIFA, Cilla Duncan, alisema tayari shirikisho hilo lenye
mamlaka ya juu kisoka ulimwenguni, limeshaanza kuchukua hatua za
kinidhamu kuhusu suala hilo.FIFA imesema inaushughulikia utata uliojitokeza kuhusu usajili wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi katika klabu za Tanzania na Tunisia.
“Tunathibitisha kwamba, kesi ya
kinidhamu (kuhusu Okwi) imeshafunguliwa. Kesi inaendelea na hivyo,
hatuwezi kueleza zaidi kuhusu kesi hiyo kwa muda huu,” alisema Duncan.
Februari 11, shirikisho hilo la kimataifa la soka liliitaka
SC Villa ya Uganda kutolea ufafanuzi sakata la uhamisho wa mshambuliaji
Emanuel Okwi katika klabu za Tanzania (Simba na Yanga) na Etoile du
Sahel ya Tunisia.Huku likiipa wiki mbili SC Villa kuwasilisha utetezi wao FIFA (kuanzia Februari 11-25, mwaka huu), shirikisho hilo lilisema imebaini dosari juu ya kumbukumbu za uhamisho wa Okwi ambazo zimekuwa na utata mwingi tangu alipohamia klabu za Simba, Yanga na Etoile du Sahel.
Shirikisho hilo lilisema kuwa, wakati Okwi anahama kutoka klabu moja kwenda nyingine, pesa pia zilikuwa zinalipwa kwa klabu ambayo Okwi alikuwa anaihama.
Lakini, FIFA ilisema kuwa takwimu zilizopo katika mfumo wake wa uhamisho wa wachezaji (TMS), zinaonyesha kwamba, Okwi alihama kutoka SC Villa kwenda SC Villa, kitu ambacho si cha kawaida, na baadaye SC Villa kwenda Yanga ilhali alikuwa mali ya Etoile du Sahel.
Okwi alihama kutoka SC Villa iliyomkuza kwenda klabu ya Simba mwaka 2010 kabla ya kuhamia klabu ya Etoile du Sahel miaka mitatu baadaye.
Mganda huyo akarudi tena kwenye klabu yake ya zamani ya SC Villa 2013, suala lililozua utata, lakini akajiunga na klabu ya Yanga mwaka huo huo.
Imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya klabu ya Villa walikuwa wanaficha ukweli wa mambo wakati wa uhamisho wa baadhi ya wachezaji.
CHANZO: NIPASHE
0 maoni:
Post a Comment