Na Baraka Mbolembole,
Nani anayejitoa kusaidia kwa
dhati mpira wa Tanzania?. TFF hakuna ‘ watendaji’, katika klabu kubwa ‘
wameshikili ‘ Mafionso’, na Chombo kilichopiganiwa sana ‘ Bodi ya Ligi’
kumejaa watu ‘ wababaishaji’ wasio na ufahamu wa kandanda. Wakati ‘ Hoja
ya msingi’ inapojitokeza, hakuna aliye tayari kujadili katika ‘ misingi
ya kimpira’. Umefikia wakati sasa wa klabu ‘ kukataa kuendeshwa katika
utumwa’ na TFF. TFF imekuwa dhaifu mno kiutendaji na wakati ipojulikana
makosa yao huwa si wazungumzaji wazuri, kwa maana kwamba mazungumzo
mengi ya msingi hugeuzwa na kuwa ‘ fimbo’ ya kuuchapa upande mwingine.
Majuzi, Ofisa mkuu wa kitengo cha
habari wa klabu ya Yanga SC, Jerry Muro aliweka wazi kuwa Simba
imefanya makosa kumchezesha kumchezesha mshambulizi Ibrahimu Ajibu
katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwa mchezaji huyo tayari
alikuwa na kadi tatu za njano na kwa mujibu wa kanuni zilizo wazi,
mchezaji anapopata kadi tatu za njano atakosa mchezo mmoja hivyo Ajibu
hakustahili kutumika katika mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 5-0,
magoli matatu ‘ Hat-trick’ yakifungwa na mshambulizi huyo kinda.
TFF ilijibu haraka kuwa, kanuni
tayari zilikuwa zimeshafiwa marekebisho huku baadadhi ya klabu tu
zilipata barua kuhusu marekebisho hayo mapya yaliyofanywa na Bodi ya
Ligi. Kanuni za sasa ni nzuri, kwa kuwa zitaruhusu klabu kumchagulia
mechi ya ‘ kumiss’ mchezaji ambaye atakuwa na kadi tatu. Simba ni kati
ya klabu zilizopata barua ya marekebisho hayo na tayari walishaitumia
dhidi ya Abdi Banda wiki mbili zilizopita wakati kiungo mwenye kadi tatu
za njano Abdi Banda alipotumika katika mchezo huo ambao Simba
walipoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Inawezekana Yanga wasiwe na ‘
hitaji la pointi za Simba kupunguzwa’ lakini kama timu ambayo inaweza
kutumia kanuni hiyo Yanga wana hoja ya msingi kwa kuwa hawana taarifa
hadi sasa. Bodi ya Ligi tayari wamekiri kuwa Yanga wana hoja ya msingi,
kuhoji ni kwanini hawajapata taarifa rasmi ya mabadiliko hayo tangu
Januari 8. Lakini katika hilo Bodi inaweza isihusike sana kwa kuwa
walitoa maagizo hayo mapema kwa Shirikisho la soka, TFF.
Kwanini Yanga hawana taarifa ya
mabadiliko hayo?. TFF imefanya uzembe mkubwa nap engine sababu muhimu
kama hii inapaswa watu wawajibike kwa kuwa hawana umakini ama hawafahamu
majukumu yao. Simbailiwasilisha barua TFF wakiomba AJIBU atumike katika
michezo dhidi ya Prisons na Yanga ili adhabu yake ifanye kazi katika
gemu dhidi ya Mtibwa Sugar, na hilo liliwezekana na Ajibu akatumika
katika mchezo huo kwa ruhusa ya TFF.
Labda pia tujiulize ni kwani
mambo yote hayo yanafanyika bila klabu nyingine kufahamu kama kuna
kanuni mpya zinatumika katika ligi?. Katika suala la Banda hakukuwa na
malalamiko, labda kwa kuwa Simba ilipoteza mchezo, lakini ili la Ajibu
limefumuka wakati zikiwa zimebaki siku chache kwa mpambano wa mahasimu
wa soka nchini Simba na Yanga. Unaweza kujiuliza ni kwanini Yanga
wamevalia ‘ njuga’ jambo hili na kupata majibu yako.
0 maoni:
Post a Comment