Mar 5, 2015

MAXIMO APATA TIMU BRAZIL

ALIYEKUWA kocha wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo (pichani juu) amefanikiwa kupata ajira mpya nchini kwao Brazil.
Maximo aliyetemwa na Yanga Desemba 19 mwaka jana akidumu kwa miezi sita, amefanikiwa kupata kibarua kipya kwa kuinoa timui ya Parana ambayo inafanya vibaya katia ligi ya jimbo moja huko Brazil.
Katika kibarua hicho Maximo anakabiliwa na shughuli pevu ya kuibakisha timu hiyo isishuke daraja wakati ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi ya huko.
Maximo alifungwa mara baada ya Yanga SC kufungwa mabao 2-0 na mahasimu, Simba SC katika mchezo wa Nani Mtani Jembe.

0 maoni:

Post a Comment