Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC itaendelea kumkosa wake Mbrazil, Andrey Coutinho katika mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC ilifikiria kumpeleka India Mbrazil huyo kwa matibabu zaidi, lakini baada ya vipimo katika hospitali moja jijini, imebainika anaweza kupona bila kwenda huko.
Kiungo huyo aliyeumia wiki iliyopita akiichezea timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City, Yanga SC ikishinda mabao 3-1 amefanyiwa vipimo leo.
Mbrazil huyo aliumia goti lake la kulia wakati akisaidia Yanga kuibuka na ushindi huo ambapo kufuatia majibu ya vipimo hivyo hataweza kusafirishwa tena India badala yake matibabu yake yatafanyika hapahapa nchini.
"Tulikuwa tunahofia kwamba anaweza kupelekwa India, alionekana kama maumivu yake ni makubwa, lakini leo tulimpeleka hospitali akiwa na daktari wetu Yomba (Richard) na kuonekana maumivu aliyonayo yatatibiwa hapahapa,"alisema bosi mmoja wa Yanga.
Kiungo huyo leo alifanikiwa kufanya mazoezi ya peke yake nje ya Uwanja kwa kukimbia taratibu katika kambi ya timu hiyo iliyopo Mbegani, Bagamoyo mkoani Pwani, lakini imethibitishwa hatacheza dhidi ya SImba SC.

Coutinho akizungumza na kocha wake, Hans van der Pluijm kambini, Mbegani leo |
Mbrazil huyo aliumia goti lake la kulia wakati akisaidia Yanga kuibuka na ushindi huo ambapo kufuatia majibu ya vipimo hivyo hataweza kusafirishwa tena India badala yake matibabu yake yatafanyika hapahapa nchini.
"Tulikuwa tunahofia kwamba anaweza kupelekwa India, alionekana kama maumivu yake ni makubwa, lakini leo tulimpeleka hospitali akiwa na daktari wetu Yomba (Richard) na kuonekana maumivu aliyonayo yatatibiwa hapahapa,"alisema bosi mmoja wa Yanga.
Kiungo huyo leo alifanikiwa kufanya mazoezi ya peke yake nje ya Uwanja kwa kukimbia taratibu katika kambi ya timu hiyo iliyopo Mbegani, Bagamoyo mkoani Pwani, lakini imethibitishwa hatacheza dhidi ya SImba SC.
0 maoni:
Post a Comment