Mar 5, 2015

MANYIKA JUNIOR YUKO FITI KUIVAA YANGA JUMAPILI

MANYIKA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA MJINI ZANZIBAR, JANA JIONI.
Kipa Peter Manyika yuko fiti yuko fiti na hivyo Kocha Goran Kopunovic atakuwa na kazi ya kuchagua, nani aanze Jumapili.


Jumapili ni siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini kwa kuwa watani wa jadi, Simba na Yanga watakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba iko kambini mjini Zanzibar wakati Yanga imechichimbia mjini Bagamoyo, kwa kifupi zote zimekimbia jijini Dar es Salaam zilipozaliwa.
Kinda huyo, yaani Manyika ambaye ni mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Yanga, Manyika Peter, alionekana yuko fiti na kufanya kazi yake kwa usafasaha mkubwa katika mazoezi ya Simba leo mjini Zanzibar.

Manyika alikuwa kivutio kutokana na alivyoifanya kazi yake kwa ufasaha, alivyokuwa akiokoa hatari kadhaa na kudaka kwa ustadi mkubwa.

Hii itamfanya kocha huyo Mserbia awe na wakati mgumu wa kuchagua katika kinda huyo au kipa mkongwe Ivo Mapunda.

Mapunda naye alionekana kuwa fiti katika mazoezi hayo yaliyokuwa ya nguvu na kasi.

05 Mar 2015
Next

0 maoni:

Post a Comment