Baada ya kumfungashia vilango
vyake aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Azama FC, Mcameroon, Joseph Omog,
Sasa wanalambalamba hao wapo kwenye mpango wa kumpatia mikoba hiyo
Stephen Keshi aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Nigeria.
Akizungumza na Shaffihdauda.com
Katibu mkuu wa Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara,
Idrissa Nasoro, Amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na Keshi,
ikiwezekana kuchukua nafasi ya Omog aliyetundikiwa daruga wiki hii.
“Tunatafuta kocha wa kusaidiana
na George Best Nsimbe, Stephen Keshi tunawasiliana naye vizuri tu,
lakini sio kwamba ndio atakuwa kocha wetu, bado tunaendelea kutafuta
kocha atakae tufaa, Hapo badaye tutaweka wazi” Amesema Idrissa Nasorro.
Juzi uongozi wa klabu ya Azam FC,
ulitangaza kuachana na kocha wake mkuu, Joseph Omog ambaye ameweka
historia ya kuwa kocha wa kwanza kuipatia timu hiyo kikombe cha Ligi kuu
ya Vodacom Tanzania Bara, ikiwa ni siku moja tu, baada ya kutua nchini
wakitokea Sudan, kucheza na El Marreikh na kutolewa kwenye michuano ya
klabu Bingwa kwa jumla ya Mabao 3-2.
Katika Mkataba wa Joseph Omog na
Azam FC kulikuwa na kipengere kilichokuwa kinasema kuwa, Omog lazima
ahakikishe anaifikisha timu hiyo katika hatua ya Makundi ya michuano ya
Klabu Bingwa zaidi ya hapo atakuwa amejivunjia Mkataba wake.
0 maoni:
Post a Comment