Kipa namba moja wa
Simba, Ivo Mapunda, amewapa onyo la mwisho mabeki wake na kuwaambia kuwa wawe
makini kwa dakika zote 90.
Kipa huyo mzoefu
amesema mabeki hao wanatakiwa kuacha kufanya makosa ya kizembe, la sivyo
ataenda mbali zaidi kwa kuwaonya kwa kuwapiga ngumi.
Katika mechi dhidi ya Stand, kipa huyo alitaka kuwapiga mabeki wake baada ya kufanya makosa mara kadhaa.
Ivo alisema kuwa
katika mechi nyingi, amekuwa akiwaona mabeki wake wakijisahau katika ukabaji na
kufanya makosa mengi ya kizembe, kitu ambacho kinaweza kuigharimu timu na kuiweka
kwenye nafasi mbaya.
“Inafikia kipindi namuonya beki aliyefanya makosa kwa kumsukuma ila naona makosa bado yanafanyika, kama wakiendelea hivi hata ngumi nitakuwa nawapiga, makosa wanayoyafanya ni ya hatari, kama wakiyafanya kwenye mechi dhidi ya timu inayojua kuyatumia vyema, basi tunaweza kufungwa kirahisi,” alisema Mapunda.
0 maoni:
Post a Comment