Mar 4, 2015

MTIBWA SUGAR IMEAMKA NA KUFANIKIWA KUITWANGA POLISI

Baada ya wakati mgumu wa kufungwa mfululizo hatimaye Mtibwa Sugar imerejea katika listi ya ushindi.


Mtibwa Sugar imeifunga Polisi Moro kwa mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Manungu mjini Turiani.

Polisi ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia Said Bahanuzi katika dakika ya 41 likadumu hadi mapumziko.

Lakini kipindi cha pili kilikuwa cha Mtibwa Sugar ambayo ilifunga mabao yake kupitia Ali Shomari katika dakika ya 53 na Said Mkopi akamaliza kazi katika dakika ya 79.

Kwa ushindi huo, sasa Mtibwa Sugar imefanikiwa kufikisha pointi 22.

0 maoni:

Post a Comment