Uongozi
wa Azam FC, umeanza juhudi za kusaka kocha msaidizi kwa ajili ya kikosi chao.
George
‘Best’ Nsimbe amepewa nafasi ya kuendelea kama kocha mkuu, huku kocha msaidizi
akitafutwa.
Habari za uhakika kutoka Azam FC zimeeleza kuwa tayari juhudi za kumsaka kocha msaidizi zimeanza.
"Kweli kuna makocha kadhaa ambao tunafanya nao mazungumzo, Best ndiye atakuwa kocha mkuu," kilieleza chanzo cha uhakika.
Best
raia wa Uganda amechukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Joseph Omog raia wa
Cameroon.
Uongozi
wa Azam FC, umeonekana kuwa na nafasi nzuri ya kumuachia Best achukue jahazi
hilo.
Omog ametimuliwa kibarua baada ya Azam FC kung’olewa na El Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2.
0 maoni:
Post a Comment