Mar 4, 2015

YANGA YAWEKA KAMBI BAGAMOYO KUSAKA POINTI TATU DHIDI YA SIMBA


Katika kuhakikisha timu yao inafanya mazoezi kwenye hali tulivu na salama, Yanga wamejificha kwenye eneo lenye msitu mkubwa huku kukiwa na siafu wengi.

Yanga wanajiwinda na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili ijayo.

Yanga yenyewe iliyoweka kambi yake kwenye hoteli moja Bagamoyo huko Pwani, inatoka umbali mrefu kuufuata uwanja ambao umezungukwa na pori kubwa huku kukiwa na milio ya ndege tu.
Kufika kwenye uwanja huo ni shughuli pevu kwani hakuna gari lolote linaloweza kufika huko zaidi ya pikipiki, hali iliyosababisha kuwa na mashabiki wachache sana.

Katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika kwenye uwanja huo, watazamaji wakubwa waliokuwa wakifuatilia mazoezi hayo yaliyoongozwa na kocha msaidizi Charles Mkwasa ni wanafunzi pekee wa chuo hicho wanaofikia 15.

Kubwa kuliko yote, uwanja huo umezungukwa na wadudu aina ya siafu ambao kama ukisimama au kukaa, lazima watakutambaa kutokana na mazingira ya msitu uliouzunguka uwanja huo.

0 maoni:

Post a Comment