BAADA ya mashabiki wa Manchester
United kuwazomea wachezaji wa timu hiyo katika mechi ya jumamosi
iliyopita dhidi paka weusi Sunderland, kocha Louis Van Gaal amekuja juu
na kuwataka wachezaji wake kutorudisha mpira mara kwa mara kwa kipa
David de gea.
Mashabiki hao waliokuwepo katika mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford, waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuonekana kukasirishwa na kuchoshwa na wachezaji wao kutofanya mashambulizi na kurudisha mpira mara kwa mara kwa kipa wa timu hiyo.
"Ninakubaliana na mashabiki, hatutakiwi kumtumia kipa mara kwa mara. Kuna muda tunapata nafasi ya kushambulia lakini hatufanyi hivyo, tunamchosha De gea " alisema Van Gaal.
Kocha huyo raia wa uholanzi,leo anakibarua kizito kukiongoza kikosi chake kitakaposhuka dimbani katika uwanja wa St.James Park kuwavaa Newcastle United ambao wamekuwa katika kiwango kizuri kwa mechi za hivi karibuni.
Manchester United inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa imejikusanyia pointi 50 katika michezo 27 waliyocheza mpaka sasa kunako ligi hiyo.

0 maoni:
Post a Comment