Licha ya kutokuwa na
kasi kama msimu uliopita, klabu ya Mbeya City imefunguka kuwa matokeo
wanayopata kwa sasa ni kawaida kwa sababu hakuna timu ambayo inaweza kushinda
kila mchezo.
Timu hiyo msimu
uliopita ilikuwa moto na kuweza kufanya vyema huku ikimaliza katika nafasi ya
tatu na kuweza kuwafunika baadhi ya wakongwe kama Simba, Coastal Union na
Kagera Sugar.
Mbeya City kwa sasa
inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 168 tu kwenye msimamo wa ligi.
Msemaji wa Mbeya
City, Mohammed Kisanda maarufu kama Dismas Ten, alisema kikosi chao kipo vizuri
lakini kwa sasa ni upepo tu unapita, mambo yatakuwa mazuri.
“Timu si kama
inafanya vibaya sana, ni matokeo ya kawaida, hakuna timu ambayo kila siku
inashinda kila mchezo, kuna sare, kufunga na kufungwa, watu walitambue hilo na
wawe na subira.
“Tunapambana
kuhakikisha tunarudi katika mstari kwa kushirikiana vyema na benchi la ufundi
na bado hatujakata tamaa, tunajipanga na tutafanya vyema japo ligi ya msimu huu
imekuwa na changamoto tofauti na ile iliyopita,” alisema Dismas.
0 maoni:
Post a Comment