Kitasa Mganda wa
Simba, Juuko Murshid, ameibuka na kuitahadharisha safu ya ushambuliaji ya Yanga
na kusema hawapati kitu.
Beki huyo ametoa
onyo hilo zikiwa ni siku chache zimebaki kabla timu hizo hazijaumana kwenye
mchezo wa Ligi Kuu Bara, Jumapili hii.
Murshid amesema
anajua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na timu zinazokutana lakini
akasisitiza kuwa, siku hiyo kazi yake ni kucheza na mafowadi wa Yanga pekee
kuhakikisha hawaleti usumbufu hata kidogo.
“Mchezo utakuwa
mgumu ila nikuhakikishie kwamba tutashinda, lakini kama nitacheza hiyo mechi
kazi yangu kubwa siku hiyo nitahakikisha hakuna fowadi wa Yanga anayeleta
usumbufu wa kufunga bao hata moja.
“Nafahamu kuwa wana rekodi na mwenendo mzuri wa kufunga katika mechi za hivi karibuni lakini hilo halinisumbui kwa kuwa safu yetu ya ulinzi ipo vizuri na tumejiandaa vya kutosha katika kupambana kuhakikisha tunaendeleza ushindi,” alisema Murshi
0 maoni:
Post a Comment