Mar 11, 2015

CANNAVARO ASHONWA NYUZI SABA

CANNAVARO BAADA YA KUSHONWA NYUZI SABA, AKIWA NA BAADHI YA WAUGUZI WALIOMHUDUMIA...
Beki ngangari wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amejiondoa kwenye kikosi hicho kitakachoivaa Platinum ya Zimbabwe.

Timu hiyo, inatarajiwa kuvaana na Platinum katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.

Cannavaro alisema amejiondoa kwenye kikosi hicho baada ya kupasuka juu ya jicho la kushoto na kusababisha ashonwe nyuzi saba.
KUMRADHI KWA PICHA: CANNAVARO WAKATI AKISHONWA...

Cannavaro alisema, nyuzi hizo alishonwa juzi Jumatatu asubuhi kwenye Hospitali ya Kilwa Road, Kurasini jijini Dar mara baada ya mechi hiyo kumalizika.

Aliongeza kuwa, hataweza kucheza kutokana na maumivu makali anayoyasikia kwenye jeraha hilo, hivyo ameona ni vyema akapumzika hadi jeraha hilo litakapopona kabisa kwa hofu ya kujitonyesha.

“Ujue nilitumia ujasiri sana kusimama na kuendelea kucheza mechi na Simba mara baada ya kugongana na mchezaji wa Simba ambaye sijamjua ni nani na nilidhani nimepasuka padogo kumbe ni pakubwa.

“Niligundua nimepasuka pakubwa mara baada ya kwenda hospitali na kugundulika jeraha ni kubwa na kutakiwa kushonwa nyuzi saba juu ya jicho langu, nilinyanyuka kuendelea kucheza kutokana na mapenzi yangu na Yanga.


“Nilitamani kucheza mechi na Platnum, lakini kutokana na jeraha hili kiukweli sitaweza kucheza, nimeona nipumzike kwa kuhofia kujitonyesha, nyuzi saba ni nyingi sana, yaani nina maumivu mara mbili ya kukosa fedha za ahadi kama tukiifunga Simba na maumivu haya niliyoyapata,” alisema Cannavaro kwa masikitiko makubwa.

0 maoni:

Post a Comment