MSHAMBULIAJI
Radamel Falcao anayesuasua tangu asajiliwe kwa mkopo Manchester United,
ameteremshwa kikosi cha pili, kinachojumuisha vijana wa umri wa miaka
21.
Falcao jana
alianzishwa katika U21 ya Manchester United iliyolazimishwa sare ya 1-1
na Tottenham Hotspur Uwanja wa Old Trafford na pia alitolewa kipindi cha
pili bila kufunga bao, ingawa alionekana kutofurahia wakati anaitwa
benchi na kocha Warren Joyce.
Katika
mchezo huo ambao, wachezaji wengine wa Man United ‘A’ Rafael, James
Wilson na kipa Victor Valdes walichezeshwa, makosa ya Joe Rothwell
yalimpa Kenny McEvoy wa Spurs nafasi ya kufunga bao la kwanza.
Rafael akaisawazishia United akitumia makosa ya kipa na kufanya sare ya 1-1.
Falcao
ambaye alikaa benchi bila kutumika juzi United ikilala 2-1 mbele ya
Arsenal, analipwa Pauni 250,000 kwa wiki na United ina hiari ya kumnunua
moja kwa moja kwa Pauni Milioni 43.2 mwishoni mwa msimu.
Kocha Louis van Gaal hajawahi kuwapeleka wachezaji timu ‘B’, labda wawe wanatoka kwenye maumivu.
Falcao aliendelea kukosa mabao ya wazi jana akiichezea Man United 'B', hadi akatolewa kipindi cha pili
0 maoni:
Post a Comment