FIGO... |
Mwanasoka nguli wa Zambia, Kalusha
Bwalya, amesema anaamini kuwa ni mapema sana kwa Luis Figo kupambana na rais wa sasa wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter.
Figo, 42, ambaye aliwahi
kuwa mchezaji bora wa duniani ni mmoja kati ya wagombea watatu wanaotaka
kuwania urais huo kwenye uchanguzi utakaofanyika Mei 29, mwaka huu.
"Luis Figo alikuwa
mchezaji mzuri sana, mchezaji wa kiwango bora zaidi duniani nilikuwa nafurahi
kila nikimwona na jezi ya Ureno.
“Nafikiri kwa mtazamo wangu
ni jambo zuri yeye kugombea, lakini naona kama vile amekwenda kwenye nafasi
kubwa sana, nafikiri haukuwa muda wake, amewahi sana,” alisema Bwalya ambaye ni
rais wa Shirikisho la Soka la Zambia.
Figo alikuwa mmoja kati ya
wachezaji mastaa wa Real Madrid wakati huo akiwa na kina Roberto Carlos, Ronaldo
de Lima pamoja na Zinedine Zidane.
Bwalya yeye alikuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 1988.
0 maoni:
Post a Comment