REAL Madrid imeitoa Schalke 04 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kufungwa mabao 4-3 nyumbani, Uwanja wa Bernabeu.
Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4, baada ya awali kushinda ugenini, Ujerumani mabao 2-0.
Mwanasoka
Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana alimpiku Lionel Messi na Raul
katika chati ya wafungaji bora wa kihistoria michuano ya Ulaya baada ya
kufunga mabao mawili katika dakika za 25 na 45. Mreno huyo sasa
anafikisha mabao 78 katika michuano ya Ulaya, akimpiku Raul aliyefunga
mabao 76 sawa na Messi.
Aidha,
Ronaldo sasa anamfikia Messi katika chati ya wafungaji wa mabao mengi
kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wote 75 kila mmoja, wakifuatiwa na Raul
mabao 71, Ruud van Nistelrooy 56 na Thierry Henry 50.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo sasa ndiye mchezaji aliyefinga mabao mengi zaidi michuano ya Ulaya
0 maoni:
Post a Comment