Kipa wa Manchester United, David de Gea anahusishwa kujiunga na Real Madrid
LOUIS
van Gaal amekiri kuwa kipa anayewindwa na Real Madrid, David de Gea
anaweza kuondoka Manchester United—lakini bosi huyo wa Old Trafford
atapambana kumbakisha.
Mapema
mwezi huu, Van Gaal alisema kipa huyo mwenye kipaji kikubwa ataongeza
mkataba, lakini kuelekea mechi ya leo dhidi ya Leicester City, amekiri
kwa mara ya kwanza kuwa anaweza kuondoka.
“Katika
mpira, kila kitu kinawezekana”, Van Gaal amesema, alipoulizwa kama
Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid watamhitaji alijibu: “Tunataka
kumbakisha”.
0 maoni:
Post a Comment