Huku
Manchester United ikitarajiwa kuchuana na Leicester katika uwanja wa
nyumbani wa Old Trafford,kiungo wa kati wa Manchester United Michael
Carrick hatoshiriki katika mechi yoyote kwa kipindi cha wiki tatu baada
ya kupata jeraha la misuli.
Ashley Young anakaribia kupona jeraha
baada ya kuumia nyuma ya goti lake,huku Jonny Evans na Chris Smalling
wakitarajiwa kushiriki.Mathew Upson huenda akarejea tena katika kikosi cha kwanza cha Leicester baada ya kupona jereha la goti alilopata kabla ya msimu kuanza.
Matty James anahudumia marufuku,Riyad Mahrez bado yuko Afrika akiichezea timu ya taifa lake ya Algeria huku Kasper Schmeichel na Chris Wood wakiwa bado wako nje na majeraha.
0 maoni:
Post a Comment