WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wanaocheza TP Mazembe, juzi Alhamisi usiku walifanya ziara ya kushitukiza kwenye hoteli ya La Rose walipoweka kambi wachezaji wa Azam.
Washambuliaji hao tegemeo wa Stars waliwasili
hotelini hapo muda wa saa mbili usiku kwa hapa Lubumbashi (saa tatu
usiku kwa Tanzania) na kuzungumza machache na wachezaji pamoja na
viongozi wa timu hiyo.
Samatta aliukosa mchezo dhidi ya Azam Jumatano
iliyopita kwani alikuwa hajarejea hapa Lubumbashi kutokea Urusi
alikokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya
CSKA Moskow.
Mkurugenzi wa Azam, Jamal Bakhresa, alipata fursa
ya kuzungumza machache na Samatta na kumshauri acheze tena msimu mmoja
na Mazembe kabla ya kuondoka kabisa kwenda kutafuta maisha Ulaya huku
pia akimtaka Ulimwengu kupambana zaidi.
“Kila mtu uwanjani alituambia kuwa tumepona
kutokana na kukosekana kwa Samatta, wanasema ungetufunga hata mabao
matatu peke yako, inaonekana wewe ni mchezaji muhimu sana hapa,” alisema
Bakhresa.
0 maoni:
Post a Comment