EMMANUEL Okwi kamili gado kuivaa
JKT Ruvu Stars katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara, kwa mujibu
wa taarifa za uhakika kutoka kambi ya Simba iliyopo Hoteli ya Ndege
Beach, kambi ya Jeshi Mbweni, jijini Dar es salaam.
Mganda huyo kipenzi cha
Wanamsimbazi jana alifanya mazoezi kikamilifu chini ya kocha mkuu Goran
Kopunovic na Mserbia huyo alisema anaendelea vizuri na anamtumia kwenye
mechi ya leo.
Okwi aliumia Januari 24 katika sare ya 1-1 baina ya Simba na Azam fc uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Beki wa kati wa Azam, Aggrey Morris alimpiga kiwiko na kuzimia uwanjani, lakini sasa yuko fiti kabisa.
Habari njema zaidi kwa Mashabiki wa Simba, beki mahiri wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy naye anacheza leo kwa asilimia zote.
Kessy hakuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichofungwa 2-1 na Mbeya City fc jumatano iliyopita.
Hata hivyo, Said Hamis Ndemla ataendelea kukaa nje kutokana na majeruhi.
Taarifa za asubuhi hii kutoka
kambi ya Simba zinaeleza kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri, kocha
amefanya nao kikao na sasa wamerejea katika saikolojia nzuri tayari
kuwavaa JKT Ruvu.
Wakati huo huo Rais wa Simba, Evans Aveva alikiri jana kuwa kufanya vibaya kwa Simba ni kutokana na uchovu wa wachezaji.
Simba walitoka kombe la
Mapinduzi ambako walicheza mechi sita mfulilizo na walirudi bara na
kwenda moja kwa moja Mtwara walikoshinda mabao 2-0 dhidi ya Ndanda,
wakarudi Dar es salaam na kutoka sare ya 1-1 na Azam fc na kufungwa na
Mbeya City katikati ya wiki hii.
0 maoni:
Post a Comment