Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara atakuwa mgeni
rasmi kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Taifa Wanawake kati ya Pwani na
Temeke itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es
Salaam.
Mechi
hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni itachezeshwa na mwamuzi wa Shirikisho la SOka la
Kimataifa (Fifa), Jonesia Rukyaa, na itaonyeshwa moja kwa moja na televisheni
ya Azam. Waamuzi wasaidizi ni Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi
Matiku wakati Kamishna ni Ingridy Kimario.
Timu
za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu
kuanzia saa 8.00 mchana. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya
Proin na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini atapata kombe na sh. milioni tatu.
0 maoni:
Post a Comment