Jan 31, 2015

NAHODHA RUVU JKT AKUBALI KIPIGO CHA SIMBA, ASEMA WATAJIPANGA



Nahodha wa Ruvu JKT, George Minja amesema kufungwa kwao mabao 2-1 dhidi ya Simba ilikuwa ni hali ya kimchezo.


Minja amesema wana imani kuwa wana imani wataweza kucheza vizuri katika mechi zijazo na kurekebisha mambo.

"Mechi ilikuwa ngumu na utaona tumeshindwa lakini ni hali ya kimchezo, lakini tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zijazo," alisema.

Simba imeifunga JKT mabao 2-1 na kupata ushindi wake wa tatu msimu huu.

0 maoni:

Post a Comment