Simba SC imeagizwa kumlipa beki Donald Mosoti Omanwa takribani
dola za Marekani 14 400 kwa kusitisha mkataba wa mchezaji huyo raia wa
Kenya mwaka jana.
Kwenye barua ambayo imeandikwa na Shirikisho la Soka duniani, FIFA, Simba imeagizwa kulipa fedha hizo kwa siku thelathini zijazo pamoja na riba ya asilimia tano kwa malipo yake kwa mujibu wa uamuzi uliyoafikiwa na benchi la majaji watatu; Thomas Grimm kutoka Uswizi, Eirik Monsen wa Norway na Zola Majavu kutoka Afrika Kusini.
“Mshitakiwa, Simba SC, afaa kumlipa mdai, Donald Mosoti Omanwa, ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, malipo bora kwa kiasi cha USD 600 pamoja na 5% kama riba kwa mwaka kutoka Desemba 12, 2013,” ulisoma ujumbe uliotiwa sahihi na katibu mkuu Jerome Valcke wa korti hiyo (Dispute Resolutions Chamber).
“Mshitakiwa pia amlipe mdai ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya taarifa ya uamuzi huu, fidia ya USD 13 800 kwa uvunjaji wa mkataba pamoja na 5% kwa mwaka riba kutoka Septemba 16, 2014hadi tarehe ya ufanisi wa malipo.”
Hii ina maana kwamba beki huyo atatia kibindoni kitita cha zaidi ya shilingi million moja pesa za Kenya na zaidi ya milioni 19 pesa za Tanzania.

0 maoni:
Post a Comment