KIUNGO
Steven Gerrard amekuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kutimiza mechi 700
kihistoria baada ya kuichezea timu hiyo jana ikishinda 1-0 dhidi ya
Bolton katika mechi ya marudio Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
Nahodha
huyo wa Liverpool, alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha
Brendan Rodgers, na kuingia kwenye orodha ya Ian Callaghan na Jamie
Carragher walioichezea pia mechi 700 klabu hiyo.
Gerrard,
ambaye maisha yae yote amecheza Liverpool tu, alifurahia mafanikio yake
hayo kwa kuvaa kiatu maalum kilichoandikwa 700 nyuma pamoja na majina
ya mabinti zake, Lilly na Lexie.
Steven Gerrard amecheza mechi ya 700 Liverpool jana
+9
Kiatu alichovaa Nahodha huyo jana, No 700 chenye majina ya mabinti zake pia, Lilly and Lexie
WALIOCHEZA MECHI NYINGI LIVERPOOL
1. Ian Callaghan 857
2. Jamie Carragher 737
3. Steven Gerrard 700*
4. Ray Clemence 665
= Emlyn Hughes 665
(bado anacheza)
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 34 alibandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa
Instagram wiki iliyopita kuelezea anavyojiandaa kwa mechi ya 700, lakini
hakuwemo kwenye kikosi kilichoifunga West Ham 2-0 Uwanja wa Anfield
mwishoni mwa wiki.
Gerrard
anaweza kubaki nafasi ya tatu kwa kucheza mechi nyingi Liverpool, nyuma
ya Callaghan aliyecheza mara 857 na Carragher michezo 737, kutokana na
kuwa na mpango wa kuhamia LA Galaxy ya Marekani akalizie soka yake huko
mwishini mwa msimu.
0 maoni:
Post a Comment