Wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022, Qatar wameonyesha kuwa tayari kumuajiri meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Josep "Pep" Guardiola i Sala.
Qatar wanatajwa kuwa katika hali ya kuhitaji kufanya kazi na meneja huyo kutokana na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi tangu akiwa na FC Barcelona ambapo alipata mafanikio makubwa kwa kutwaa zaidi ya mataji kumi kwa kipindi kifupi.
Hata hivyo bado haijaelezwa viongozi wa shirikisho la soka nchini Qatar watakamilisha mpango huo lini, licha ya Guardiola kuendelea na mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa Ujerumani kwa sasa.
Taarifa kutoka huko mashariki ya kati ilipo nchi ya Qatar, zinaeleza kwamba meneja huyo anapigiwa upatu wa kuajiriwa mapema kwa ajili ya kupata nafasi ya kukaa pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo
kabla ya kuingia katika mikakati ya kuwania ubingwa wa dunia wa mwaka 2022.
Endapo ndoto za Qatar zitakuwa kweli, itakua ni mara ya kwanza kwa Guardiola kufundisha timu ya taifa tangu alipoanza shughuli za ukocha mwaka 2007, kwa kuinoa timu B ya FC Barcelona.
0 maoni:
Post a Comment