Na Augustino Mabalwe
Kocha wa klabu ya Mwadui Jamhuri
kihwelo “Julio” ametua katika klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa
mkopo mpaka mwisho wa msimu huu ambapo atakuwa klabuni hapo kama kocha
msaidizi.
Imeripotiwa kuwa kocha huyo
amechukua uamuzi huo kutokana na urafiki wake wa karibu na klabu
hiyo,pia analengo la kuinua kiwango cha timu hiyo kinachoonekana kuyumba
msimu huu.
Coastal Union ambayo iko chini ya
kocha mkenya James Nandwa imekuwa ikisuasua kunako ligi kuu Tanzania
bara na kwa sasa inashika nafasi 7 ikiwa na pointi 19 katika ligi hiyo.
Julio amekuwa kocha tishio nchini
na sasa ameipandisha daraja timu ya Mwadui na kutwaa ubingwa wa ligi
daraja la kwanza baada ya kuitandika African sports katika mchezo wa
fainali uliopigwa jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex huko
Chamanzi jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Post a Comment