Adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa kiungo wa Chelsea Nemanja Matic imepunguzwa hadi mechi mbili. Mchezaji huyo atakosa mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi siku ya Jumapili dhidi ya Tottenham. Tume huru ya udhibiti ya Chama cha soka cha England FA ilishikilia adhabu, baada ya rufaa kukatwa na Chelsea siku ya Jumanne. Matic, 26, alioneshwa kadi nyekundu siku ya Jumamosi katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley, baada ya kukasirishwa na jinsi Ashley Barnes alivyomkwatua. Katika taarifa iliyotolewa, Chelsea wamesema "wamesikitishwa na kuhuzunishwa" na hatua ya Matic kutumikia adhabu. Mbali na kukosa mechi ya fainali ya Jumapili itakayochezwa Wembley, Matic pia atakosa mchezo dhidi ya West Ham United wa Jumatano Machi 4.
0 maoni:
Post a Comment