AZAM FC ni klabu inayojifunza
na kuendeleza pale inapofikia kwa misimu minne sasa tofauti na klabu
kongwe za Simba na Yanga ambazo hupanda na kushuka.
ANGALIA TAKWIMU HIZI
2010/2011-Simba walishika
nafasi ya pili kwa pointi 49, huku Yanga wakichukua ubingwa kwa pointi
49, lakini walibebwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Walifunga magoli 32, walifungwa magoli 7, tofauti ilikuwa magoli 25.
Simba walifunga magoli 40, walifungwa 17, tofauti ya magoli ilikuwa 23.
2011/2012-Simba walitwaa
ubingwa wa ligi kuu kwa kujikusanyia pointi 62, huku Azam fc wakishika
nafasi ya pili kwa pointi 56, Yanga wakashika nafasi ya tatu kwa pointi
49.
Kumbuka msimu uliopita wakati huo, Yanga walikuwa mabingwa na Simba walikuwa wa pili.
2012/2013- Yanga walichukua
ubingwa kwa pointi 60, Azam fc wakashika nafasi ya pili kwa pointi 54,
Simba wakawa wa tatu kwa pointi 45.
Hapa utaona Yanga kutoka nafasi
ya tatu msimu uliopita wakati huo akachukua ubingwa, Simba akashika
nafasi ya tatu kutoka kuwa bingwa. Azam akaendelea kubakia nafasi ya
pili kwa msimu wa pili mfululizo.
2013/2014- Azam fc walitwaa
ubingwa kwa pointi 62, Yanga wakashika nafasi ya pili kwa pointi 56,
Simba nafasi ya nne kwa pointi 38.
Utagundua kuwa Azam
waliendeleza walipoishia, kutoka nafasi ya pili mfululizo na kutwaa
ubingwa, Simba wakashuka zaidi mpaka nafasi ya nne wakiwapisha Mbeya
City nafasi ya tatu waliojikusanyia pointi 49.
Mpira wa miguu ni takwimu, hapa Azam fc wamekuwa bora kuliko Simba na Yan
0 maoni:
Post a Comment