“Niwaambie ukweli mashabiki
wangu, kila mtu anayeniunga mkono ni kama familia yangu, kila shabiki
wangu ni kama mtoto wangu, kila shabiki ni mtu muhimu kwangu, kila
shabiki ni muhimu kwa Simba, lakini kila shabiki lazima aelewe kitu hiki
muhimu;
“Timu hii ni changa sana, timu
hii inahitaji muda, sisemi kuwa tunahitaji miaka kumi, hapana!
Tunahitaji muda, nilikuja nimechelewa, nikiwa na Matola tunajaribu sana
kuiboresha timu hii, lakini timu hii ina presha, tunawapa presha kubwa
wachezaji wangu kila wiki, lakini wachezaji wangu hawana uzoefu
kwasababu ni wachanga”
Wakati fulani tunacheza vizuri,
wakati fulani tunaanguka, wakati fulani tunashinda, kila shabiki lazima
aelewe kitu hiki, hata sare, lazima wawape wachezaji wangu nguvu kwa
ajili ya mechi ijayo, unapoanza kupiga kelele..aaaah! nini? Aaaah! mechi
inayofuata inakuwa hatari zaidi kwa mchezaji mchanga kwasababu hana
uzoefu wa kuwaza mechi iliyopita, pia hana uwezo binafsi wa kujijenga na
kuongeza morali ya mchezo ujao”.
“Kwa timu yangu, kocha Goran
anaahidi, kila mechi, kila mazoezi, ninafanya kazi kwa asilimia mia
moja, wachezaji wangu kila wanapocheza mechi wanacheza kwa juhudi,
wanacheza kwa ajili ya Simba, lakini wakati fulani hatushindi kila
mechi”
Maneno haya yamezungumzwa na
kocha mkuu wa Simba Sc, Goran Kopunovic wakati huu kikosi chake
kikijiandaa kuivaa Prisons uwanja wa Taifa, Dar es salaam katika mechi
ya ligi kuu Tanzania bara.
Mwishoni mwa wiki iliyopita,
Simba walifungwa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga
0 maoni:
Post a Comment