Mar 20, 2015

AIBU HII HAIJAWAHI KUTOKEA ENGLAND!

EVERTON imekuwa timu ya mwisho ya England na Uingereza kwa ujumla kutolewa katika michuano ya Ulaya, baada ya kufungwa mabao 5-2 Dynamo Kiev usiku wa Alhamisi.
Everton inatolewa katika hatua ya 32 Bora kwa jumla ya mabao 6-4, baada ya awali kushinda 2-1 nyumbani.
Romelu Lukaku gave his side hope but his equaliser proved to be a false dawn for Everton, who subsequently conceded four
Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Everton ikilala 5-2 mbele ya wenyeji Dynamo Kien nchini Ukraine usiku wa Alhamisi

KLABU ZA ENGLAND ZILIVYOVURUNDA ULAYA MSIMU HUU

Liverpool, (February 26, Europa League last 32): Baada ya kushika nafasi ya tatu katika makundi Ligi ya Mabinhgwa, LIverpool ilitolewa na Besiktas kwa penalti.
Tottenham (February 26, Europa League last 32): Ilitolewa na Fiorentina kwa kufungwa 2-0 mechi ya marudiano.
Chelsea (March 11, Champions League last 16): Came a cropper against 10-man Paris Saint-Germain in extra time.
Arsenal (March 17, Champions League last 16): Ilitolewa kwa mabao ya ugenini licha ya kushinda  2-0 mjini Monaco.
Manchester City (March 18, Champions League last 16): Mabingwa wa England walifungwa nyumbani na ugenini na Barcelona.
Everton (March 19, Europa League last 32): Ilifungwa 5-2 na Kiev nchini Ukraine.
Hii inakuwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya England, nchi hiyo inakosa timu katika hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ulaya.
Hiyo inafuatia kutolewa kwa timu za Arsenal, Manchester City na Chelsea katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Man City juzi ilifungwa 1-0 na Barcelona, bao pekee la Ivan Rakitic dakika ya 31, akimalizia krosi ya Lionel Messi na kutolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 3-1, baada ya awali kufungwa 2-1 England.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero alikosa penalti dakika ya 78 ambayo iliokolewa na kipa Marc-Andre ter Stegen. Penalti hiyo ilitolewa baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Gerard Pique.
Arsenal ilitolewa kwa sheria ya mabao ya ugenini, baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Monaco nchini Ufaransa na kufanya sare ya jumla ya 3-3, kufuatia awali kufungwa 3-1 nyumbani.
Chelsea ilitupwa nje kwa mabao ya ugenini pia, baada ya sare ya jumla ya 3-3 na PSG ya Ufaransa. Hiyo ilifuatia Chelsea kutoa sare ya 2-2 nyumbani baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 ugenini na timu hiyo ya Ufaransa.


0 maoni:

Post a Comment