Shirikisho la
Soka Ulaya (Uefa) leo limekamilisha upangaji wa ratiba ya mechi za robo fainali
huku Real Madrid ikipewa Atletico Madrid.
Wapinzani hao
wakubwa kutoka nchini Hispania walicheza fainali ya mwaka jana ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya na Real Madrid kuibuka na ushindi, tena katika dakika za mwisho.
Barcelona wao
watakutana na kiboko ya Chelsea, yaani PSG.
FC Porto
wanakutana na mzigo wa Bayern Munich na Juventus wao watapambana na AS Monaco
ya Ufaransa iliyoitoa Arsenal.
Mechi:
PSG Vs Barcelona
Atletico Madrid
Vs Madrid
Porto Vs Bayern
Juve Vs Monaco
0 maoni:
Post a Comment