Mar 20, 2015

CANNAVARO AREJEA MZIGONI, YU TAYARI KWA MGAMBO KESHO

CANNAVARO (WA TATU KUSHOTO) AKIWA NA WENZAKE WAKIJIFUA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI MJINI TANGA, LEO.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amerejea mazoezini na kuungana na wenzake mjini Tanfa.

Cannavaro ambaye alishonwa nyuzi saba baada ya kupasuka usoni wakati wa mechi ya watani wao Simba, leo amejifua na wenzake kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Akionekana yuko fiti, Cannavaro amejifua na wenzake hali inayoonyesha ana nafasi ya kuitumikia Yanga itakapokuwa ikiivaa Mgambo, kesho.

Yanga ipo Tanga, tayari kuwavaa Mgambo ambao mechi iliyopita waliishinda Simba kwa mabao 2-0.

0 maoni:

Post a Comment