Mshambuliaji wa klabu ya Simba
pamoja na Timu ya Taifa ya Uganda, Dan Sserunkuma, amefunguka ya moyoni
kuhusiana na ushirikina na kusema kuwa, Hajawahi kuambiwa na uongozi wa
timu juu ya kutumia maswala hayo licha yakuwa Imani yake hairuhusu
Ushirikina.
Nyota huyo ambaye alikuwa ni
mfungaji bora wa ligi kuu ya Kenya kwa misimu miwili iliyopita mfululizo
akiwa Gor Mahia, Amesema hayo leo kupitia akaunti yake ya Twitter na
kusema kuwa bado anaipenda Simba wala hafikilii kuondoka Msimbazi.
“Napenda kusema yafuatayo,
Ninafuraha kuwa Simba, Sitaki kuondoka Simba, Sijawahi kulalamika
kubaguliwa Simba, Sijawahi kulazimishwa na uongozi kutumia Uchawi kama
ambavyo siamini” Ameandika Sserunkuma kwenye mtandao wa kijamii wa
Twitter.
0 maoni:
Post a Comment