Kocha wa timu ya taifa ya England
Roy Hodgson amesema ingeshangaza sana kama mchezaji kinda wa klabu ya
Tottenham Harry Kane asingejumuishwa katika kikosi cha Nchi hiyo
kinachotarajiwa kumenyana na Lithuaniana na Italy.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 21, ni miongoni mwa wachezaji 24 wa kikosi cha
England ambacho kimetajwa na Hodgson kucheza dhidi ya Lithuania mchezo
ambao utapigwa katika dimba la Wembley mnamo march ,27 mwaka huu
kwaajili ya mechi za kufuzu katika mashindano katika mataifa ya Ulaya
yanayotarajia kufanyika mwakani. Kikosi hicho pia kinatarajia kuumana na
Italy katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa mjini Turin huko Italy
tarehe 31 mwezi huu.
0 maoni:
Post a Comment