Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba anashangazwa na habari za upotoshaji zinazoenezwa kuhusu kanuni mpya ya adhabu za kadi, kwamba klabu yao ilipotoshwa.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Dar es Salaam, Hans Poppe amesema watu wamekuwa wakieneza uvumi kwamba kanuni ya kumuombea mchezaji mwenye kadi kucheza mchezo unaofuata ili akose mwingine baadaye haikupitishwa.Hans Poppe amesema huo si ukweli, kwani kanuni hiyo ilipitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake cha Februari 8, mwaka huu.
Amesema baada ya hapo, klabu zilisambaziwa barua iliyosainiwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa kujulishwa juu ya kanuni hiyo mpya na Simba SC walifikishiwa waraka huo.
“Sisi tulipoipata hiyo barua, tukatumia fursa hiyo kwa kuwaombea wachezaji wetu ambao walikuwa kwenye mazingira hayo, ajabu sasa watu wanaanza kuleta mizengwe,”amesema Hans Poppe.
Kumekuwa na madai kwamba, kanuni hiyo ilijadiliwa tu katika kikao cha Kamati ya Utendaji ili ianze kutumika msimu ujao, lakini Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ambaye pia ni kiongozi wa Simba SC akaenda kuipotosha klabu yake.
Wazi anayelengwa hapo ni Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye ndiye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Hans Poppe amesema; “Sisi hatukuambiwa na Kaburu, tuliletewa barua na TFF na nakala tunayo,”amesema.
Simba SC ilitumia fursa hiyo mara mbili, kwanza kwa mchezaji Abdi Banda iliyemtumia katika mchezo dhidi ya Stand United mjini Shinyanya, japo ilifungwa 1-0 na baadaye Ibrahim Hajibu katika mchezo dhidi ya Prisons.
Simba SC iliifunga Prisons 5-0 na tangu hapo kumekuwa kuna malalamiko juu ya Hajibu kucheza akiwa ana kadi tatu za njano, licha ya klabu hiyo kutoa ufafanuzi wa kutumia fursa ya kanuni mpya.

Hans Poppe akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga kulia |

0 maoni:
Post a Comment