Na Vincent Malouda, NAIROBI
WAKALA wa straika la Simba SC Dan Sserunkuma, Ken Joseph, amesisitiza kuwa mteja wake yungali mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwaka 2016.
Kumekuwepo na tetesi kuwa raia huyo wa Uganda tayari amewaandikia viongozi wa Simba barua akielezea azma ya kusitisha mkataba wake mwishoni mwa msimu huu kufuatia kutoridhishwa kwake kukalishwa kwenye benchi.
Sserunkuma hajarejea kambini baada ya kupewa ruhusa ya muda kushughulikia maswala ya kifamilia. Alitarajiwa kurejea Dar Jumamosi iliyopita baada ya kuondokea kwao Uganda pindi tu Simba ilipolazwa na Yanga taifa Machi 8.
“Naweza kukuthibitishia kwamba Dan Sserunkuma ni mchezaji wa Simba SC. Dan alipewa ruhusa ya siku chache na klabu kwenda nyumbani kisha arejee kambini. Ninachojua ni kwamba hakuna tatizo lolote kati ya Sserunkuma na Simba wala hajaniambia jambo lolote kuhusu kuondoka klabu hiyo, “ wakala huyo mzawa wa Uingereza na mwenye uraia wa Nigeria aliliambia BIN ZUBEIRY.
“Pia ijulikane kuwa Sserunkuma ni mchezaji mwenye hadhi ya juu jinsi wasifu kazi wake unavyosoma.”
Sserunkuma alisajiliwa Simba mwezi Desemba kutokea Gor Mahia ya Kenya alipomaliza mfungaji bora wa ligi kuu Kenya kwa magoli 16 na hadi kufikia sasa amecheka na nyavu mara tatu tu.
Amewahi kuzichezea Express FC na Victors FC za Uganda na vile vile Nairobi City Stars ya Kenya na pia kufanya majaribio nchini Armenia na Denmark.

Dan Sseunkuma kulia akiichezea Simba SC katika Ligi Kuu |

0 maoni:
Post a Comment