Mar 12, 2015

BAYERN MUNICH YAIADHIBU SHAKHTAR DONETSK 7-0


bayern-munich-celebration_3275483Na. Richard Bakana
Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa barani Ulaya, Klabu ya Bayern Munich  usiku huu wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuwafumua Shakhtar Donetsk kwa jumla ya mabao 7-0.
Mabao ya Bayern Munich yametupiwa kambani na Müller  katika Dakika ya 4 kwa mkwaju wa penati ikiwa ni bao la kwanza kabla ya dakika ya  51 ya mchezo huo kuiandikia timu yake bao la nne.
Naye Boateng aliiandikia timu yake bao la pili katika dakika ya 34, Ribéry akifunga goli la tatu katika dakika ya 49, Badstuber  alifunga bao la tano katika Dakika ya 63, Lewandowski akitupia la sita kunako dakika ya 75 kabla ya Götze kumaliza kazi kwa kufunga bao la saba katika dakika ya 87.
Hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Bayern Munich wamefanikiwa kuondoka kifua mbele kwa jumla ya mabao 7-0.
Kwa matokeo hayo sasa Wajermani hao wanakuwa wametinga katika hatua ya Robo fainali ya Klabu bingwa Ulaya kwa ushindi huo mnono.Thomas MullerThomas Muller akifunga bao lake usiku huu.

0 maoni:

Post a Comment